SHINIKIZO LA DAMU NI TATIZO LENYE IDADI KUBWA YA WAGONJWA KWA ASILIMIA 70 TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Ivan Edmund kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Philips Pharmaceuticals Tanzania Ltd. akitoa dawa kwa mwananchi aliyekutwa na tatizo la moyo mara baada ya kupata matibabu wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya jinsi gani unaweza kuepuka kupata magonjwa ya moyo kwa wananchi waliofika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo wilya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale wali...