RAIS SAMIA AANZA NA WAANDISHI WA HABARI
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akila kiapo cha uaminifu   Na John Mapepele, Dodoma Tanzania imeandika historia ya kuwa na Rais mwanamke wa kwanza kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi tarehe 19 Machi, 2021 kushika wadhifa huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Mhe, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021.   Kwa Mujibu wa ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kijiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana namaradhi ya mwili au  kushindwa  kutekeleza kazi za rais, basi  Makamu wa Rais ataapishwa  na atakuwa Rais kwa muda  uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.   Mara baada ya kula kiapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na majon...