YAKUBU- VYUO VIKUU ENDELEENI KUANDAA MATAMASHA
  Na. John Mapepele Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ametoa wito  kwa vyuo vikuu nchini vinavyofundisha sanaa kuandaa matamashaa  ya utamaduni ili kuibua vipaji vitakavyoleta ajira kwa vijana. Yakubu ameyasema  haya  leo  Januari 29, 2022 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed  Mchengerwa wakati wa kilele cha tamasha la  sanaa la kuadhimisha miaka 60 ya Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam toka kuanzishwa kwake. Amefafanua kwamba matamasha haya yanasaidia kuibua vipaji na kuendeleza utamaduni wa taifa letu. Aidha, amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa nafasi ya washindi watatu katika tamasha hili kushiriki kwenye tamasha kubwa la kitaifa la Serengeti litakalofanyika  Dodoma mapema mwezi Machi 2022. Amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa  kuunga  mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuendeleza Utamaduni na dira yake ya 2061 na mikakati yake ya kuimaris...