RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaipongeza Timu ya Taifa ya Tembo Warriors kwa kufuzu kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu linalotarajiwa kufunguliwa Septemba 30, 2022 na kuitaka kutanguliza uzalendo na kujituma ili warudi na Kombe nyumbani. Akizungumza kwa njia ya simu kupitia kwa Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania ipo pamoja na wao katika kila hatua na ndio maana Rais ameridhia viongozi wa Wizara kuambatana nao katika fainali hizo. “Rais na Serikali yenu ipo pamoja na nyinyi, nendeni mkalipiganie Taifa, onesheni uzalendo na kuhakikisha mnarudi na Kimbe nchini na hiyo itakuwa ni zawadi kwake Mhe. Rais na Tanzania kwa ujumla”’ amefafanua Mhe. Mchengerwa. Aidha ameahidi zawadi nono kwa timu hiyo ikiwemo shilingi milioni 40 endapo watafuzu robo fainali, shilingi milioni 80 wakifuzu kucheza nusu fainali na shilingi milioni 100 waki...