RAIS DKT. SAMIA, WAZIRI MCHENGERWA WATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA SHUKRAN TUZO ZA FILAMU 2022
Na John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa wametunukiwa Tuzo maalum ya shukrani kwa mchango wao katika kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Sanaa. Tuzo hizo zimetolewa kwenye kilele cha utoaji wa Tuzo za Filamu 2022 uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kituo cha Kimataifa cha Mkutano Arusha, AICC. Awali kabla ya kukabidhi Tuzo hizo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiagho Kilonzo amesema Mhe. Mchengerwa amechaguliwa kwa kuzingatia mchango wake mkubwa alioufanya katika kipindi kifupi tangu achaguliwe kusimamia sekta hiyo ambayo inaongoza kwenye kuchangia ukuaji wa uchumi. Amesema maelekezo ambayo amekuwa akiyatoa na kuyasimamia yamesaidia kukuza Sekta hiyo kwa kiwango kikubwa. "Ni kutokana na maelekezo thabiti ya Mheshimiwa Waziri ndiyo maana leo tunashuhudia kufanyika kwa mafanikio makubwa utoaji wa Tuzo wa msimu wa pili" amefafanua Kilonzo Tuzo ya Mhe. Rais ilikabidhi...