Mhe. Mchengerwa atembelea miundombinu ya Michezo Uingereza
Na John Mapepele, Leicester Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametembelea miundombinu ya michezo nchini Uingereza na kufanya mazungumzo na wamiliki wake lengo likiwa ni kuboresha miundombinu ya michezo nchini. Katika ziara hiyo aliyoifanya Julai 30, 2022, Mhe. Mchengerwa ametembelea kiwanja cha King Power na St Mary’s kinachomilikiwa na klabu ya Southampton na kujionea miundombinu mbalimbali ya michezo na kujifunza namna bora ya kuiendeleza na usimamizi wa miundombinu hiyo. “Tumejifunza mambo mambo mengi makubwa ambayo sisi pia tunaweza kuyaiga na kuyaboresha kutoka kwa wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye anga ya michezo na sisi tukapiga hatua ya haraka” amefafanua Mhe. Mchengerwa Akiwa kwenye ziara hiyo Mhe. Mchengerwa alipata fursa ya kushuhudia fainali za kombe la ngao ya jamii mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa ...