Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Simba kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi timu ya Orlando Pirates Aprili 17, 2022 kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam. Pongezi hizi ameendelea kuzitoa leo baada ya zile alizotoa jana mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo. Ikumbukwe kuwa Mhe. Mchengerwa jana aliwaongoza maelfu ya watanzania kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan kuishangilia Simba katika uwanja wa Mkapa hatimaye ikatwaa ubingwa huo. Asubuhi kabla ya mechi hiyo, Mhe. Mchengerwa baada ya kumaliza kushiriki mashindano makubwa ya Qur'an barani Afrika yaliyofanyika kwenye uwanja huo huo wa Mkapa, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wake Said Yakubu alitoa wito kwa watanzania kujitokeza kuja kuishangilia Simba katika mechi hiyo iliyochezwa kuanzia saa moja usiku ili ishinde. Ubingwa wa Simba ulipatikana kupitia kwa beki kisiki Sho...
Comments
Post a Comment