Dunia yaitazama Royal Tour kupitia mhadhara wa Gurudev

 


Na John Mapepele

Mamilioni ya watu usiku wa kuamkia leo Agosti 26, 2022 wameitazama  Tanzania  kupitia Filamu ya Royal Tour katika mhadhara maalum uliofanywa na balozi wa amani duniani Gurudev Sri Sri Ravishankar.

Gurudev anasakikika  kuwa na wafuasi zaidi ya milioni mia tano duniani kote ambao   humfuatilia  Kila anapotembea dunia kote kuhubiri amani, furaha na upendo.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa ndiyo aliyewaongoza watanzania  kushiriki kwenye mhadhara huo uliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiambapana na Katibu Mkuu wa wizara yake Dkt Hassan Abbasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Royal Tour.

Katika ukumbi huo ambao ulifurika kwa mamia ya watu na wengi kukosa mahali pa kuketi Filamu hiyo ilichezwa na kuonesha vivutio mbalimbali vya Tanzania ambapo hatimaye ilishangiliwa sana  huku timu ya vyombo vya ndani na nje vilivyoongozana na Mhubiri huyo vikirusha  tukio hilo mbashara.


Katika tukio hilo Gurudev alisisitiza mahubiri ya kulinda  amani na kufanya mazoezi ambayo yatawapatia furaha na upendo na kufafanua kuwa mazoezi yanaleta afya njema kwa wanadamu.

Akiongea katika tukio hilo, mwenyeji wa mgeni huyo. Mhe Mohamed Mchengerwa amemwomba Mhubiri huyo kutumia lugha ya Kiswahili popote anapokwenda duniani kwa kuwa imekuwa miongoni mwa  lugha inakua duniani na kusikilizwa na watu wengi 

Amesema ujio wake umekuwa katika kipindi mwafaka wakati Serikali ya awamu ya sita ikiwa imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta zake za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwapa wananchi wake furaha, amani na upendo baina yao.



 Ameongeza kuwa wizara yake ndiyo wizara yenye nguvu laini inayosaidia kwa kiasi kikubwa nchi kupiga hatua za kimaendeleo baada ya kuwapa furaha.

Amefafanua kuwa tafiti zinaonesha kuwa, matatizo mengi ya kiafya ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo na migogoro ni kutokana na kukosekana kwa furaha na amani. 

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa ni kisiwa cha amani duniani pia kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na muasisi wa taifa letu, mwalim Julius Nyerere na awamu zote za uongozi hadi uongozi wa sasa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan 

 Amemwelezea Rais  Samia Suluhu Hassan kuwa ni Rais wa kwanza mwanamke katika nchi za Afrika mashariki ambaye amefanya  Mambo makubwa katika kipindi chake akiwa madaeakani.


Aidha amesema Tanzania na  India imekuwa na mahusiano mazuri  ya kibiashara na kiutamaduni kwa kipindi kirefu  ttangu miaka ya 1400 zikiunganishwa na Bahari ya Hindi.


Comments

Popular posts from this blog

VIONGOZI WA DINI MKOANI SINGIDA WAJA NA MAAZIMIO SABA UCHAGUZI MKUU

Wadau wapongeza MIF kwa kusaidia mtoto wa kike Zanzibar, wajitokeza kuichangia

Hongereni Simba- Mhe, Mchengerwa