Waziri Mchengerwa atoa wito kwa jeshi kuwa na timu ya soka.
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa majeshi kuanzisha timu ya soka itakayoshiriki ligi kuu nchini ili kuongeza ushindani na mvuto wa ligi. Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2022 kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jakob John Mkunda katika uwanja wa Gofu wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mashindano ya Gofu ya NBC Lugalo Patron Trophy 2022. Amefafanua kuwa majeshi yamekuwa na historia ya kutoa mchango mkubwa ambapo ameelezea kwamba wachezaji wengi wanaoshinda katika mashindano mengi wanatoka kwenye majeshi. Aidha amesema kutokana na nidhamu iliyojengeka kwenye majeshi anaimani kuwa jeshi linauwezo wa kuanzisha timu hiyo ambayo itakuwa miongoni mwa timu tishio ndani na nje ya nchi yetu. Amesifu juhudi zinafanywa na jeshi katika kuanzisha klabu ya gofu na miundombinu ya michezo huo Dar es Salaam na Dodoma na kuruhusu raia kutumia ambapo a...